22 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Kagere ampa mzuka Rayvanny

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KITENDO cha mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, kushangilia kwa staili ya wimbo wa Tetema wa msanii wa lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Ray­mond Mwakyusa ‘Rayvanny’, kimempandisha mzuka mkali huyo wa Bongo Fleva na kuitungia wimbo Taifa Stars.

Kagere amekuwa akishangilia kwa staili ya wimbo huo wa Tetema ambao unatamba kwa sasa hasa pale anapofunga bao.

Akizungumza na MTANZANIA juzi wakati wa maandalizi ya video ya kuisapoti Taifa Stars, msanii huyo alisema ameona ni jambo zuri kuitungia wimbo timu hiyo ya Taifa, hasa katika kipindi hiki wanachoelekea kucheza na Uganda.

“Nimeona ni jambo jema kuja kuisapoti Taifa Stars, lakini pia napata furaha kuona wachezaji wengi wanacheza wimbo wangu wa Tetema pale wanapokuwa wanafunga kitendo hiki kimezidi kunipa raha zaidi,” alisema.

Alisema wimbo huo ambao wanauandaa kuisapoti Stars, utaongeza hamasa kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuisapoti timu hiyo kesho.

Taifa Stars wanatarajia kucheza na Uganda kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles