Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
Bao pekee la Medie Kagere la dakika ya 70, limeipa Simba pointi tatu mbele ya Dodoma Jiji kwenye Uwanja wa Jamhuri na kuwafanya mabingwa watetezi hao kukaa kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ukiachana na alama tatu timu yake ilizochukua, ushundi huo umewafanya wachezaji wa Dodoma Jiji kukosa kitita cha fedha sh milioni 15 walizokuwa wameahidiwa endapo wangeshinda mechi hiyo na milioni 10 kama wangepata sare.
Kutokana ushindi huo Simba imefikisha pointi nne baada ya mchezo uliopita kutoka suluhu na Biashara United kwenye Uwanja wa Karume, Mara.
Mchezo mwingine uliopigwa leo Oktoka Mosi, Ruvu Shooting imefanyikiwa kuwafunga Biashara United bao 1-0 lililofungwa na Rashid Juma kwenye Uwanja wa Karume.