24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Kagere aendelea kusota Rwanda

Na WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM

SERIKALI ya Rwanda, imeongeza muda kwa wananchi wake kukaa ndani na mipaka kufungwa hadi Aprili 30, mwaka huu kutokana na janga la virusi vya corona, hivyo kuondoa matumaini ya mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, kurejea nchini Tanzania kwa sasa.

Awali baada ya ugonjwa wa Corona kuingia nchini humo, Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame, alitoa agizo la wananchi wake kukaa ndani hadi Machi 21, lakini baadae ikaongezwa tena siku zilizotarajia kumalizika leo.

Hata hivyo, kutokana na wagonjwa kuzidi kuongezeka, serikali ya Rwanda, imeamua kuongeza siku za kuendelea kukaa ndani na mipaka kufungwa hadi Aprili 30, ili kuangalia hali ya kusambaa kwa virusi hivyo.

Kitendo cha mipaka kufungwa kwa watu kutoka na kuingia ndani ya nchi hiyo kutamfanya Kagere ashindwe kuondoka ukizingatia na Tanzania nayo imefunga mipaka yake.

Hivi karibuni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Senzo Mbata, alisema angetamani nyota wake waliopo nje ya nchi wapate ruhusa ya kurejea nchini mapema ili waweze kukaa karantini kwa siku 14.

Tofauti na Kagere, wachezaji wengine  wa Simba waliokwama katika nchi zao kutokana na janga hili la Corona, ni Clatous Chama (Zambia), Luis Miquissone (Msumbiji), Francis Kahata (Kenya) na Sharaf Shiboub (Sudan)

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles