22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Kagera wahimizwa kuchanja chanjo ya corona

Na Renatha Kipaka, Bukoba

WANANCHI mkoani Kagera wametakiwa kuacha tamaduni zilizo zoeleka ili kuepuka maambukizi ya virusi vya corona.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Mkao huo, Profesa Faustine Kamzora wakati wa uzinduzi wa chanjo uliofanyika katika hospitali ya Rufaa iliyopo mjini Bukoba.

Amesema tangu miaka ya nyuma watu walichoma chanjo na hakukuwa na madhara ikiwa nipamoja na chanjo ya bega.

“Watu tumechanjwa tukiwa wadogo lakini sikuwahi kusikia mtu amepata madhara, sasa hata katika chanjo hii tuamini nikawaida tu kama zilivyo chanjo zingine ili watu wachanjwe tusonge mbele,” amesema Kamzora.

Ameongeza kuwa katika Mkoa wa Kagera kutakuwa na vituo 18 vya kuchanjia ikiwa katika Manispaa ya Bukoba ambako kutakuwa na vituo viwili ambapo kituo kimoja kutakuwa hospitali ya Mkoa na Zamuzamu.

“Ndugu zangu mimi ni Mzee ninachanjwa hapa ili nipate kinga ya Covid-19, hivyo basi niwaombe wazee wenzanzgu mjitokeze kwa wingi kuchanja tusisubiri hadi tuzidiwe,” amesema Kamzora.

Kwa upande wake Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kiraini amewataka watu kubadilika kulingana na hali na kwamba waache tamaduni za kwenda kwenye msiba na kurundikana na badala yake watanyike.

Kiraini amesema kuwa kama Kuna uwezekano watu wanapo maliza kuwazika wapendwa wao watawanyike ili wabakie watu wa familia husika kuondokana na ugonjwa kuwa na kasi zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles