22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Kagame, Sall kuzungumza na wajasiriamali 5,000

ABUJA, NIGERIA

MARAIS Paul Kagame wa Rwanda na Macky Sall wa Senegel wanatarajia kuzungumza na wajasilramali 5,000 kutoka mataifa 54 ya Afrika wakati wa jukwaa la kila mwaka la ujasiriamali Julai 26 mwaka huu.

Likiwa linasubiriwa kwa hamu kubwa, jukwaa hilo la tano na la siku mbili linaloandaliwa na Shirika la Tony Elumelu Foundation (TEF) litafanyika kwenye Hoteli ya Transcorp Hilton   mjini hapa.

Tukio hilo ni hitimisho ya Programu ya Ujasiriamali ya kila mwaka ya Tony Elumelu ambayo mwaka huu imefunza na kuchagua vijana 3,000 kati ya waombaji zaidi ya 216,000 kutoka kona zote za Afrika.

Tukio hilo linatoa fursa adimu kwa vijana wa kike na kiume kutoka mataifa ya Afrika kukutana, kujifunza na kujenga mtandao ya  biashara ndani na nje ya Afrika.

Pia ni fursa nzuri kwa viongozi wa siasa na watunga sera kukutana, kukabiliana uso kwa uso na kizazi kipya cha viongozi wa  biashara  ambao watabadili na kustawisha uchumi wa Afrika.

Marais Kagame na Sall, wataungana na Tony O. Elumelu, mwasisi wa TEF na Mwenyekiti wa Heirs Holdings na United Bank for Africa (UBA) katika majadiliano ya wazi na washiriki.

Kujumuisha marais katika jukwaa hilo kunaruhusu wajasiriamali wa Afrika wanaoshiriki kongamano hilo kujadiliana na kuchangamana kwa karibu na viongozi wa siasa  ambao watatoa ushuhuda wa jukumu muhimu  ambalo serikali inaweza kushiriki katika kuchocchea ukuaji na kuchochea hamasa ya biashara.

Yatakayojiri ni pamoja ni jopo la majadiliano na wazungumzaji wakuu na wataalamu wa sekta kutoka Afrika na nje ya bara  ambao watatoa elimu na uzoefu kwa washiriki kuimarisha ujuzi wao na kuboresha stadi zao.

Majukwaa yaliyotangulia yaliongozwa na viongozi wa Afrika kama vile Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo.

Wengine ni Waziri Mkuu wa zamani wa Benin na Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa TEF, Lionel Zinsou, Makamu Rais wa Nigeria, Profesa Yemi Osinbajo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles