26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kagaigai aagiza baraza la madiwani kujadili hoja 66 za CAG

Na Upendo Mosha,Mwanga

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Zefrin Lubuva, kutenga siku moja ya Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kujadili jumla ya hoja 66 za ukaguzi zilizodumu kwa zaidi ya miaka nane .

Mkuu huyo wa mkoa alitoa agizo hilo Juni 14, 2021 wakati akizungumza katika kikao maalumu cha baraza la madiwani cha halmashauri ya wilaya ya Mwanga cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere.

Amesema halmashauri hiyo kushindwa kujibu hoja za ukaguzi 66 tangu mwaka 2013 ni uzembe na kwamba ipo haja ya Mkurugenzi huyo kuandaa kikao maalumu cha kujadili hoja hizo kwa lengo la kulinda mapato na fedha za serikali.

“Hoja hizi nyingi ni za Mwaka 2013 na 2014 kutozikamilisja mpaka sasa naweza kusema ni uzembe maana mnavyozidi kurundika hoja hizi ndio zinavyozidi kuwa nyingi lazima inapokuja hoja mzijibu na msonge mbelee,”amesema.

Aidha, amesema kuna umuhimu mkubwa wa kujadiliwa kwa hoja hizo kwa lengo la kupata ufumbuzi na kulinda fedha za serikali na mapato ya halmashauri.

“Mfano ya nimeangalia hoja ya kutokatwa kodi ya Sh milion tano kwa wakandarasi, majibu ya menejimenti yanasema jambo hilo linatarajiwa kufutwa kwenye vikao vya kufuta hoja nikajiuliza inawezekanaje kufuta hoja bila kujiridhisha juu ya jambo hili…sio sawa na hamuitendei haki serikali,” amesema Kagaigai.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya madiwani hao walisema kumekuwa na utendaji usioridhisha kwa watendaji wa halmashauri hiyo jambo ambalo limekuwa likisababisha baadhi ya hoja kutojibiwa na kufanyiwa kazi.

Diwani wa Kata ya Kivisini, Ziadi Mwalimu amesema suala la utawala bora kwa watendaji wa halmahauri hiyo limekuwa ni changamoto na kwamba magizo yanayotolewa na madiwani yamekuwa yakipuuzwa na kuchangia kutojibiwa kwa hoja 66 za ukaguzi toka mwaka 2013.

“Kuna tabia ya watumishi kulindana ikitokea mtu anataka kushughulia hoja hizi anawekewa mapingamizi na wengine kuamishwa halmashauri hii haiheshimu maagizo ya madiwani…tunaomba mwenyekiti usimame kwenye nafasi yako,” amesema Yasta Msuya ambaye ni diwani wakata ya Mwanga.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Zefrin Lubuva amesema atahakikisha kikao hicho maalumu cha kujadili hoja hizo Julai 5, 2021 jambo ambalo litatoa mwanya wa madiwani kujadili kwa kina hoja moja moja na kupatiwa ufumbuzi.

Naye, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Muhamedi Hassan amewaagiza watendaji wa halmashauri kuzingatia ushauri unaotolewa na baraza la madiwani katika kushughulia hoja hizo za ukaguzi kwa wakati jambo ambalo litaepusha msuguano na migogoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles