30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kafulila: Hatukujenga stendi kuleta usumubufu kwa wananchi 

*Ipigilia msumari uamuzi wa DC, CCM

*Asema utabaki kama ulivyo

Na Derick Milton, Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila amesema uamuzi wa kuamisha magari madogo ya abiria (Mchomoko) kutoka stendi kuu ya mabasi (Somanda) katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani humo na kuyapeleka eneo la soko kuu ilipokuwepo stendi ya zamani utabaki kama ulivyo.

Amesema Serikali haikujenga stendi hiyo kwa ajili ya kuleta usumbufu kwa wananchi, bali ni kwa ajili ya kusaidia wanananchi wake ukiwa ndiyo msingi mkuu wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa huo, wakati akielezea mafanikio ya mkoa huo ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu.

Kauli hiyo ya Kafulila imekuja zikiwa zimepita siku nne tu zimepita tangu madiwani wa halmashauri hiyo kupinga uamuzi uliofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Lupakisyo Kapange na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya wa kuhmisha magari hayo.

Katika kikao chao cha Baraza la Halmashuari kilichofanyika Machi 15, 2022, madiwani hao walilalamikia uamuzi huo kwa madai kuwa umesababisha mapato ya halmashauri kushuka na ulifanywa kisiasa zaidi na bila wao kushirikishwa.

“Katika taarifa yetu ya kamati ya fedha tuliyoiwasilisha leo kwenye kikao cha baraza la madiwani tumeeleza ni namna gani maamuzi ya viongozi wetu yanavyoendelea kuiumiza halmashauri…mapato yetu kwa sasa yameshuka na yataendelea kushuka kama hatutachukua hatua za haraka za kurudisha gari ndogo ndani ya standi kuu…,” alisema mmoja wa madiwani hao Kija Bulenya.

Kwenye kikao chake na Waandishi wa habari leo Jumamosi Machi 19, 2022 akizungumzia mwaka mmoja wa mafanikio ya serikali ya awamu ya sita, Kafulila amesema msingi wa maamuzi yaliyofanywa kuamisha magari hayo ni kupunguza usumbufu kwa wananchi.

“Uamuzi wa kuondoa magari madogo ulishafanyika na utabaki kuwa hivyo hivyo …jambo la msingi wa maamuzi hayo ni kupunguza bughuza au usumbufu kwa wananch.

“Serikali ilijenga stendi hiyo kwa ajili ya kusaidia wananchi …na msingi wa kuwepo kwa stendi hiyo ni wananchi watumie kwa mapenzi na siyo shuruti na hivyo adhima ya serikali ya awamu ya sita ni kuleta maendeleo kwa watu,” amesema Kafulila.

Amesema kuwa suala la kupungua mapato, wao kama viongozi watakaa na kuangalia namna bora ya stendi kuendelea kufanya vizuri ili kuweza kuongeza mapato ya halmashuari.

“Kwa kweli hatuwezi kukusanya mapato kwa ajili ya kusumbua watu, suala la mapato tutakaa tuangalie njia bora ya kuweza kuifanya stendi hiyo ifanye vizuri zaidi ya hapa,” amesema Kafulila.

Akizungumzia mafaniko ya Mkoa ndani ya Mwaka mmoja wa Rais Samia, amesema miradi yote ya maendeleo ambayo serikali imeleta fedha zake inaendelea kutekelezwa na itakamilika ndani uliopangwa.

Amesema kuwa katika sekta ya maji, miradi yote 32 inayotekelezwa ndani ya mkoa pindi itakapokamilika itawezesha hali ya upatikanaji wa maji kwa kiwango cha asilimia 90 mjini na vijijini.

Sekta ya miundombinu ya barabara, amesema mkoa umesaini mikataba 58 yenye thamani ya Sh bilioni 11 kwa ajili ya ujenzi na karabati wa miundombinu ya barabara za vijijini na mjini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles