25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Kafulila afungua kesi Mahakama Kuu Tabora

escrowNa Murugwa Thomas, Tabora

ALIYEKUWA mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila kupitia Chama cha NCCR – Mageuzi, amefungua kesi Mahakam Kuu Kanda ya Tabora kupinga ushindi wa Hasna Mwillima wa Chama Cha Mapindunzi (CCM), aliyetangazwa mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Kafulila amewasilisha pingamizi hilo jana kupitia kwa wakili wake, Daniel Lumenyela, huku akiwa ameambatanisha nakala za fomu za matokeo ya kura ya vituo vyote 382 vya jimbo hilo ambazo zilisainiwa na mawakala wa vyama vyote zinazoonesha alishinda uchaguzi huo.

Akiwa mahakamani hapo, umati wa wanachama wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ulifurika tangu majira ya saa mbili asubuhi.

Akizungumza mara baada ya kuwasilisha pingamizi hilo, Kafulila alisema ameiomba mahakama ipitie nyaraka hizo na kisha imtangaze yeye kuwa mshindi wa uchaguzi wa jimbo hilo.

Alidai msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Reuben Mfune, alipewa shinikizo na viongozi wa Serikali amtangaze mgombea wa CCM, Hasna Mwilima, kuwa mshindi kwa kura 34,000 dhidi ya kura 32,000 alizopewa yeye.

Kafulila alisema toka siku hiyo Oktoba 28, mwaka huu yalipotangazwa matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo chini ya ulinzi mkali, msimamizi huyo bado hajaonekana hadharani.

Hata hivyo awali matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo yalikuwa yakitarajiwa kutangazwa Oktoba 27, mwaka huu lakini alisitisha utangazaji huo kwa madai kuwa ameshauriwa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuagizwa kusitisha zoezi la utangazaji hadi hapo baadaye.

Msimamizi huyo alikaririwa kuwa uamuzi wake huo wa kuwasiliana na ngazi za juu ulitokana na mgombea wa CCM Hasna Mwilima kugomea matokeo baada ya zoezi la kuhakiki kukamilika wakiwa pamoja.

“Haki ya wapiga kura wa Jimbo la Kigoma Kusini itapatikana lakini kinachofanyika ni kunichelewesha kunitangaza mimi kuwa mbunge,”  alisema Kafulila.

Alibainisha katika kile kinachoonyesha ni kuficha unyang’anyi waliofanya hata nakala za majumuisho ya matokeo ya kura za wagombea hawakupewa wala kuonyeshwa fomu zake.

Kwa upande wake Wakili Lunyemela anayemwakilisha Kafulila katika shauri hilo alisema uchaguzi mzima haukuwa na utata na ndiyo maana mteja wake anadai mahakamani kutangazwa kuwa ndiye mshindi halali wa jimbo hilo.

“Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo alichofanya ni kuchukua matokeo ya kura ya mteja wake na kumpa aliyekuwa mgombea wa CCM Hasna Mwillima na ndiyo maana walilazimisha kuwepo kwa ulinzi mkali ili watangaze matokeo batili,” alisema.

Lunyemela alisema sheria ya uchaguzi na 343 imeweka vigezo muhimu vya kumpata na kumtangaza mshindi wa uchaguzi ikionyesha wazi kuwa aliyepata kura nyigi ndiye anastaili kuwa mshindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,211FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles