24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

KADCO yajipanga kuongeza idadi ya abiria KIA

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

KAMPUNI ya Uendelezaji na Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KADCO) imetaja mikakati iliyonayo ni pamoja na kuongeza idadi ya abiria na kukarabati eneo la uwanja.

Pia imesema imetoa gawio la Sh bilioni 2.9 kwa Serikali kuanzia mwaka 2016 hadi 2019.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Oktoba 11, mwaka huu jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa bajeti na mwelekeo wa kampuni hiyo hiyo kwa mwaka 2022-2023.

Mwakatobe ameitaja mikakati ambayo wanayo ni kuongeza idadi ya abiria na kukarabati eneo la uwanja ili kuchukua magari 200 kutoka magari 83 yanayoweza kuchukuliwa kwa sasa.

Amesema mpaka sasa mkataba wa ukarabati wa ujenzi huo umeshasainiwa na hivi karibuni ujenzi utaanza na utagharimu Sh bilioni 2.7.

Amesema  tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo imelipa kodi kwa serikali zaidi ya Sh bilioni 6.

Amesema kampuni hiyo pia imetoa gawio kwa Serikali Sh bilioni 3 ambapo mwaka 2016/17 Kampuni ilitoa Sh milioni 555 mwaka 2017/18 ilitoa Sh milioni 583 na mwaka 2018/19 iliigawia serikali Sh bilioni moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles