30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Kada atoa vifaa vya Sh mil 2

Gustaphu Haule- Pwani

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Kibaha mkoani Pwani,  Aboubakary Alawi,amekipiga tafu chama chake kwa kutoa vifaa mbalimbali.

Vifaa hivyo, ni pamoja na kompyuta moja, printa na bendera 110 vyenye thamani zaidi ya  Sh milioni 2.

Alawi alitoa vifaa ili kusaidia na kurahisisha utendaji wa shughuli za kila siku katika  ofisi ya CCM ya Kibaha Mjini jambo ambalo limesaidia kupunguza  gharama  kwa chama kutumia pesa katika kukamilisha shughuli zake.

Alikabidhi vifaa hivyo jana kwa Katibu wa CCM Kibaha Mjini, Hafidh Luambano hafla ambayo ilifanyika ofisini kwa katibu na kushuhudiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa.

Pia alikuwapo Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), Judith Mruge,Katibu wa Itikadi na Uenezi Kibaha Mjini, Elias Masenga na Katibu wa Vijana, Amina Makona.

Akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Alawi alisema katika maisha yake amelelewa na chama hicho na hata mafanikio aliyopata yametokana ndani ya chama.

Alisema ametoa vifaa hivyo ili kurudisha heshima kwa chama chake namna ambavyo kilimlea na kumtunza tangu akiwa mdogo.

“Mimi ni mzaliwa wa Kibaha ambaye nimelelewa na CCM,nimesoma Shule ya Msingi Mailimoja,nikaenda Sekondari ya Kibaha,baadae nikarudi kufundisha Kibaha na mpaka sasa naishi  hapa… kwa hiyo mafanikio yangu yametokana na chama changu,”alisema Alawi

Alisema katika maisha yake, aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika chama na jumuiya zake, ikiwemo mwenyekiti wa wazazi naa anafahamu namna chama kinavyofanyakazi vizuri na hata kusaidia wananchi.

Alisema awamu hii, chama kimebahatika kupata mwenyekiti mzuri ambaye ni Rais Dk . John Magufuli, ni vema watu waliopo ngazi za chini wajitokeze kushirikiana naye ili kukiimarisha zaidi.

Naye Luambano alimshukuru Alawi kwa kujitolea  kutatua changamoto hiyo, kwani ameonyesha mfano mzuri katika kukiimarisha chama.

Alisema vifaa hivyo, vimekuja wakati muafaka na vitatumika kwa malengo ya kufanyakazi za chama kwakuwa awali walilazimika kutumia pesa nyingi kwenda steshenari za nje.

“Kwa niaba ya kamati nzima ya Siasa ya Kibaha Mjini, tunakushukuru kwa kujitoa kwako kuisaidia ofisi vitendeakazi hivi, ni kweli uliandika barua kwetu na bahati nzuri kamati ilikubali na ikakupa majibu kwa barua, leo (jana), umetekeleza adhma yako,”alisema Luambano

Alisema wapo tayari kumpokea mwana chama  yeyote mwenye dhamira ya kukijenga chama kwa kufuata utaratibu kwakuwa sio dhambi kwa mtu mwenye kujitolea kwa faida ya wengi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,348FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles