31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Kabudi: Wanaofungisha ndoa wawekwe kwenye mfumo wa elekroniki

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

SERIKALI imeagiza Wakala wa Usajili,Ufilisi na Udhamini (RITA), kuhakikisha viongozi wa dini wanaofungisha ndoa wote wanasajiliwa kwenye mtandao wa E elekrtoniki.

Akizingumza wakati wa siku ya usajili wa matukio ya binadamu na takwimu barani Afrika, Dar es Salaam leo, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema hatua hiyo itasaidia mno Wakala kupata idadi kamili ambayo itawezesha Serikali kupata takwimu sahihi za watu wanaofunga ndoa.

Amesema wafungaji ndoa wengi nchini hawapeleki takwimu sahihi na kwa wakati serikalini.
Kuhusu umuhimu wa Usajili, Waziri Kabudi aliuagiza Wakala kuongeza kasi ya kutoa elimu kwa wananchi ili watambua umuhimu wa kupata vyeti.

Amesema Kama wakipata elimu, watambua umuhimu huo kwa sababu cheti hicho no muhimu kutokana ana kuhitajika sehemu nyingi.

Amesema cheti za kifo kinahitajika wakati wa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu wanapokwenda kupata mikopo na kusema wamefiwa, huombwa cheti. Amesema hatua hiyo ni muhimu itasaidia mno kupunguza kero kwa wananchi.

Aliagiza Wakala kuitisha kikao ambacho kitajumuisha viongozi wanaohusika na masuala ya ndoa, ili wapate maelekezo ya Serikali.

Kuhusu usajili wa watoto, amesema Tanzania imepiga hatua kubwa ambapo Sasa usajili umefika asilimia 55 kutoka asilimia 13 ya mwaka 2012.

Amesema mpaka sasa watoto zaidi ya milioni 6.5 wamesajiliwa maeneo mbalimbali nchini.
Amesema Wakala umeboresha huduma hiyo ambayo mwakani wakati wa sensa ya watu na makazi itatoa taswira Hali ya watoto waliopo nchini.

Amesema Wakala unafanya kazi nzuri mno, kwa sababu umeweka mifumo mizuri ikiwamo ya simu janja ambazo zimesaidia kufanikisha usajili.

Kaimu Kabidhi Wasiii Mkuu na Kaimu Mkurugenzi wa Haki za Kisheria, Lina Msanga amesema Tanzania imepiga hatua kubwa barani Afrika.

Amesema mafanikio hayo yamefanya Tanzania ichaguliwe kuwa kinara kwa kwenda mataifa mengi kutoka elimu juu ya masuala ya usajili wa vizazi na vifo.

Amesema mafanikio hayo yamefanya Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Emmy Hudson ameteuliwa kuwa kiongozi wa masuala ya usajili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles