26.9 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Kabudi : Wajasiriamali jifunzeni teknolojia mpya Nanenane

 ASHURA KAZINJA

WAKULIMA, wafugaji, wavuvi na wajasiliamali, wametakiwa kutumia maonesho ya Nanenane kujifunza teknolojia mpya na fursa mbalimbali kujiendeleza kiuchumi.

Wito huo, ulitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi wakati ufunguzi wa maonesho ya 27 ya Nanenane ya Kanda ya Mashariki yenye kauli mbiu ‘Kwa maendeleo ya kilimo, uvuvi na mifugo chagua viongozi bora 2020’ yaliyofanyika viwanja vya Mwalimu Nyerere mkoani Morogoro.

Waziri Kabudi aliwashauri washiriki hao kutumia teknolojia na fursa iliyopo kuzalisha kwa tija katika kilimo, mifugo na uvuvi itakayowasaidia kuzalisha kwa wingi ili kuwezesha kupata malighafi kwa ajili ya viwanda.

Alisema ni vema maonesho yajayo yakatumika pia katika kuwafundisha wakulima namna ya kulima mimea na miti dawa kutokana na kuwa na fursa kubwa katika nchi za nje, ikiwemo Indonesia, Thailand na Madagascar.

“Maonesho yajayo tusionyeshe mazao mengine tu peke yake, bali tuonyeshe pia namna ya kulima miti dawa na mimea dawa, tulime miti na mimea dawa kwani inafursa kubwa nchi za nje ikiwemo Madagascar, Indonesia na Thailand,” alisema. 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro, alisema iwapo wakulima, wafugaji, wavuvi na wajasiliamali watajifunza na kuzingatia na kuyatekeleza yote waliojifunza watainuka kiuchumi.

Alikemea vikali tabia ya uharibifu wa mazingira kwa Mkoa wa Morogoro na kuutaka uongozi husika kuchukua hatua kali dhidi ya wale wote watakao bainika kufanya,bila kuwaonea aibu na kusema ni jukumu la kanda ya mashariki kuhakikisha wanalinda mazingira.

“Morogoro ni mkoa wenye maji na mito mingi, tayari dalili za kuharibu mazingira zimeanza kuonekana, tumeanza tabia mbaya ya kujenga juu ya milima, tuepuke kulima na kupeleka mifugo katika vyanzo vya maji, wahusika tusioneane aibu tuambiane ukweli,” alisema.

Alisema mbali na kuwapo changamoto ya corona iliyosababisha maandalizi ya maonesho hayo kuchelewa lakini idadi ya washirika imeongezeka kutoka washirika 514 mwaka jana mpaka 561 mwaka huu.

Aliwataka wakulima wa zao la korosho kuhakikisha wanatumia dawa pamoja na kusafisha mashamba yao, kutokana na zao hilo kuathiriwa na mvua na hivyo kuwepo changangamoto ya uzalishaji.

“Kilimo cha korosho katika kanda ya mashariki kiliathiriwa na mvua, rai yangu wakulima wasafishe mashamba yao,kwani korosho zilioza kutokana na kuanguka kwenye maji na kuoza” alisemaNdikilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles