24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kabendera bado hali tete, apewa siku saba kuelezea alichofanyiwa na daktari

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeamuru mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera (39), ambaye hali yake ya kiafya bado ni tete, arudi mahakamani baada ya siku saba ili kupata taarifa ya matibabu.

Uamuzi huo ulitolewa leo saa tatu asubuhi wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa katika mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Mahakama ilimpa nafasi Kabendera kuelezea maumivu anayosikia ambapo akijieleza alidai hali ya kushindwa kupumua usiku bado inaendelea na siku nane zilizopita alisikia maumivu makali mguu wa kulia, maumivu makali katika mfupa ndani ya paja hali inayomfanya akose usingizi.

Anadai alionana na daktari jana akamwambia kulikuwa na ugeni anamsikiliza kesho lakini mara ya mwisho aliomuona Alhamisi iliyopita na tiba aliyopata ni kupimwa damu na kuchomwa sindano tatu za maumivu.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu aliamuru arudi Septemba 18 ili aje kueleza kitu gani alichofanyiwa baada ya kuonana na daktari.

Awali, Wakili wa Kabendera, Jebra Kambole aliendelea kusisitiza kwamba afya ya mteja wake inaendelea kutetereka, mguu wa kulia umepooza na hajapata tiba sahihi wanaomba apelekwe katika hospitali za Serikali ili afanyiwe vipimo. Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Kabendera anakabiliwa na na mashtaka matatu ambapo shtaka la kwanza ni kwamba kati ya Januari mwaka 2015 na Julai 2019 maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam Kabendera na wengine ambao hawapo mahakamani anadaiwa alitoa msaada kwenye genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia fedha.

Inadaiwa shtaka la pili, mshtakiwa anadaiwa kukwepa kodi, inadaiwa kati ya Januari, 2015 na Julai 2019 maeneo mbalimbali ya DAR es Salaam bila sababu za msingi alikwepa kulipa kodi Sh 173,247,047.02 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika shtaka la tatu la kutakatisha fedha, inadaiwa katika tarehe hizo mshtakiwa alitakatisha kiasi hicho cha fedha huku akijua zimetokana na zao la kusaidia genge la uhalifu na kukwepa kodi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles