23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

K-Finance yaleta mkopo wa gari la ndoto yako

Na Tunu Nassor, Dar es Salaam

Taasisi ya Fedha ya K-Finance imekuja na suluhisho la changamoto ya usafiri  hasa wakazi mjini kwa kuwezesha kumiliki gari kwa kulipa nusu ya gharama na fedha zinazobaki kumaliziwa taratibu kama marejesho ya mkopo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkopo huo, jijini Dar es Salaam leo Mei 7, mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa K-Finance Judith Minzi amesema lengo ni kutatua changamoto ya usafiri hasa kwa wakazi wa mijini.

“Tunajua kuwa usafiri wa umma hasa kwa wakazi wa mijini umekuwa hautoshelezi na kusababisha wengi kuchelewa katika shughuli zao za kila siku na K-Finance tumeliona hilo na tumeleta mradi mpya wa kuwasaidia wananchi kumiliki magari yao binafsi,” amesema Judith.

Judith amesema mradi huo pia utasaidia kwa walioagiza magari na kushindwa kutoa bandarini kutokana na kukosa fedha.

Amesema pia mkopo huo utawasaidia wasafirishaji kuweza  kuongeza idadi ya magari kwa mfumo wa kulipia nusu bei.

“Tumeingia makubaliano na kampuni zinazoagiza magari nje ya nchi hivyo kumwezesha mteja kuchagua gari analotaka katika yadi zao ama kuagiza kwenye mtandao,” amesema.

Ameongeza kuwa  kwa kushirikiana na kampuni hizo itasaidia kumfikishia mteja gari lake bila udanganyifu ikiwamo wizi wa vipuli, kubadilishiwa gari ama kuletewa gari lenye rangi tofauti na lililoagizwa.

Aidha Judith amewaalika mawakala waaminifu na wenye uzoefu wa kuagiza magari kushirikiana nao ili kuweza kusaidiana katika kutatua changamoto ya wanajamii wengi kuweza kumiliki gari nchini.

“Tunajinasibu kwa kutatua changamoto za kifedha zilizopo katika jamii na tumekuwa tukifanya tafiti kwanza ndipo tunaandaa mradi,” amesema Judith.

K-Finance ni taasisi ya kifedha inayotoa mikopo yenye suluhisho na huduma wezeshi za kifedha, pale mtu anapohitaji kukamilisha ada za shule, zabuni mbalimbali, fedha(mtaji) wa kuendesha biashara na mikopo binafsi na hivi karibuni usafiri  ambapo inapatikana kwa kutembelea tovuti ya yao ya www.kfinance.co.tz

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles