22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

JWTZ, TRA WAKAMATA MALI ZA MAGENDO

Mizigo iliyokamatwa na maofi sa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ikishushwa kutoka katika jahazi lililokuwa limebeba bidhaa za magendo maeneo ya Kunduchi, Dar es Salaam jana.
Mizigo iliyokamatwa na maofi sa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ikishushwa kutoka katika jahazi lililokuwa limebeba bidhaa za magendo maeneo ya Kunduchi, Dar es Salaam jana.

Na KOKU DAVID-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wamelazimika kutumia silaha za moto kuwakama watu saba waliokuwa katika jahazi lililobeba bidhaa za magendo eneo la Kunduchi, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, kiongozi wa kitengo cha doria wa TRA, Elias Sipemba, alisema kwa siku nne mfululizo walifanya doria maeneo ya Bagamoyo na Kunduchi na kufanikiwa kuwakamata watu hao wakiwa na majahazi manne yaliyokuwa yamebeba bidhaa mbalimbali za magendo.

Alisema majahazi mawili yaliyokamatwa Bagamoyo yalikuwa yakitokea Zanzibar na yalipitia bandarini. Yalikuwa yamebeba mafuta ya kula madumu 870 ya lita 20, magunia matano ya sukari ya kg 50, redio tatu, majokofu manne, spika mbili za redio, amira boksi 10 na boksi nne za betri za redio.

“Nahodha aliyekuwa akiendesha jahazi mojawapo kati ya yale manne ni Mrisho Salehe Mrisho (18) ambaye alikataa kutii amri ya kusimama na ndipo wakalazimika kutumia silaha za moto kumsimamisha.

“Kijana huyo alikaidi amri ya kusimama, alikuwa akilikimbiza jahazi kuelekea upande ambao kulikuwa na kundi kubwa la watu, ambao inasadikika walikuwa wenzao, na walikuwa wameshika silaha mbalimbali za jadi,” alisema Sipemba.

Aliongeza kuwa majahazi mengine mawili yaliyokamatwa Kunduchi yalitokea Unguja na yalikuwa yamebeba mafuta ya kula, mafuta ya taa majokofu, belo nane za kanga ambavyo vilipakiwa katika bandari bubu ya Uzini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles