23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Jux atamani mtoto wa kike

Na GLORY MLAY

MKALI wa muziki wa RnB nchini, Juma Jux, amesema kuwa anatamani kupata mtoto wa kike kwa sababu anataka amlee kwenye mazingira ya kujitegemea zaidi.

Jux amesema anaamini mtoto wa kike ana uwezo wa kuwekeza na kusaidia watu wengi, hivyo anatamani kuwa na mtoto wa kike.

“Ninaomba mtoto wangu wakwanza awe wakike, ila anaweza akawa hata wa pili kama nitaanza na wakiume, nitamlea katika akili ili aweze kujitegemea zaidi, naamini kwenye kuwekeza kwa mwanamke ili ajitegemee kwa sababu mwanamke anaweza kusaidia wengi.

“Mwanamke ambaye anaweza kujitegemea atakuwa vizuri kwenye maisha kuliko anayemtegemea mtu, hivyo hicho ndiyo kitu ambacho nakiangaliaga, hata kwa mtu ambaye nakuwa naye kwenye uhusiano naangalia kama ana uwezo wa kujitegemea na hata kama hawezi nitamtengenezea mazingira aweze kujitegemea bila mimi,” alisema Jux.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,636FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles