27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

Juve wamrudisha Kean

BAADA ya miaka miwili tangu walipomuuza, Juventus wamemsajili kwa mara nyingine mshambuliaji wa kimataifa wa Italia, Moise Kean.

Kean (21), aliyezichezea Everton na PSG, amerudi Juventus kwa makubaliano ya mkopo wa misimu miwili, ingawa mkataba wake una kipengele kinachoiruhusu klabu hiyo kumsajili moja kwa moja.

Nyota huyo aliibuliwa na Juventus aliyojiunga nayo akiwa na umri wa miaka 11 na mara ya kwanza kuingia timu ya wakubwa ni msimu wa 2018-2019 alipofunga mabao saba 7 katika mechi 17.

Baadaye, Juve walimuuza kwenda Everton lakini huko alichemsha na ndipo alipopelekwa kwa mkopo PSG alikoweza kufunga mabao 17 katika mechi 41.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles