22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Justine Kussaga: Siku ya Msanii iwe daraja la mafanikio

Justine Kussaga
Justine Kussaga

NA SALMA MPELI,

WASANII wa kazi mbalimbali nchini wameshauriwa kutumia maadhimisho ya Siku ya Msanii yanayotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu kama darajal la mafanikio yao.

Hayo yalisemwa na Mratibu wa siku hiyo, Justine Kussaga, akiongeza kwamba wasanii wa Tanzania wanatakiwa kuitumia siku hiyo kujifunza ili waendeleze sanaa zao.

“Siku ya msanii inahusisha mambo mbalimbali hivyo ni muhimu kwa wasanii waitumie kama sehemu yao ya mafanikio kwa kazi zao na hata kujifunza vitu tofauti katika muziki, maonyesho ya ufundi na maigizo,” alisema Kussaga.

Siku hiyo huadhimishwa kila mwaka ambapo licha ya mafunzo tuzo mbalimbali hutolewa kwa wasanii mbalimbali kutokana na mchango wao kwa jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles