Justin Bieber kumpigania Billie Eilish

0
978

New York, Marekani

BAADA ya Justin Bieber kuachia albamu mpya inayojulikana kwa jina la ‘Changes’ msanii huyo ameweka wazi mipango yake ya kutaka kuhamishia nguvu zake kwa mwanadada Billie Eilish.

Bieber amedai anataka kujitolea kumsaidia mrembo huyo mwenye umri wa miaka 18 katika muziki wake ili aje kuwa bora kwenye ushindani.

“Namuona jinsi anavyokuja kuwa staa wa muziki duniani, ana kipaji cha hali ya juu, nimeona kama atakosa mtu wa kumsaidia basi kipaji chake kitapotea, nataka kujitolea kwa ajili yake pia lazima nimlinde,” alisema msanii huyo.

Bieber anaamini wasanii wengi wanasaidiwa na ndio maana wanafika mbali, hata yeye alipata msaada kutoka kwa wasanii mbalimbali kama vile Usher Raymond.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here