24.6 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Julio aponda usajili wachezaji wa kigeni

Jamhuri Kihwelu ‘Julio’
Jamhuri Kihwelu ‘Julio’

NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Mwadui FC, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, amesema hababaishwi na usajili wa wachezaji wa kimataifa unaofanywa na baadhi ya klabu zitakazoshiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao na kudai kuwa ana uwezo wa kupata wachezaji wazawa wenye viwango vya juu zaidi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Julio alisema anaamini wapo wachezaji wazawa wenye uwezo kwani baadhi yao viwango vinalingana na ambao wanasajiliwa kutoka nje ya nchi.

“Wachezaji wa nje ambao nakubali viwango vyao ni Thabani Kamusoko, Donald Ngoma na Haruna Niyonzima wa Yanga pamoja na Kipre Tchetche wa Azam FC, lakini wengine wana uwezo wa kawaida,” alisema.

Julio aliyeipandisha Mwadui Ligi Kuu na kuiwezesha kubaki msimu uliopita, alisema atafanya usajili wa wachezaji wazawa wenye uwezo ambao anaamini watakiimarisha kikosi na kuongeza ushindani msimu ujao.

Akizungumzia tetesi za kutaka kumsajili kiungo aliyetemwa na Yanga, Salum Telela, Julio alikiri kufanya naye mazungumzo na kudai kilichobaki ni mchezaji huyo kufanya uamuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles