24.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Julio aponda ratiba Kombe la FA

pic+kiweluNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

KOCHA wa timu ya Mwadui FC, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, ameiponda ratiba ya Kombe la FA hatua ya 16 bora iliyotolewa juzi na Shirikisho la Soka nchini (TFF), akidai inazipendelea timu kubwa ili kupenya na kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho.

Kwenye ratiba hiyo, timu ya Mwadui imepangwa kucheza na Rhino Rangers, mchezo utakaochezwa Februari 27 katika Uwanja wa Mwadui.

Akizungumza na MTANZANIA, Julio alisema mara kadhaa timu kubwa zimekuwa zikibebwa na ratiba hiyo na kuongeza kuwa lengo ni kuzisaidia kucheza kimataifa.

“Ukiangalia kwa makini utaona timu zote kubwa zimepangiwa na timu ndogo, ambazo hazina ushindani licha ya mashindano haya kimataifa hayaangalii ukubwa au udogo wa timu.

“Kitu muhimu katika michuano hii ni kuhakikisha tunapata ushindi, hata kama tutapangiwa na timu ya aina gani hadi tupate nafasi ya kuwakilisha kimataifa,” alisema Julio.

Julio alieleza hatodharau timu yoyote atakayopangiwa nayo licha ya udhaifu wa ratiba hiyo, atapambana ili kuthibitisha ubora wa timu yake.

“Mzunguko wa kwanza nilifanikiwa kupata ushindi dhidi ya Stand United, safari hii wamenipangia na Rhino Rangers pia nitashinda hadi nipate nafasi ya kuwakilisha kimataifa kwenye michuano hii,” alisema Julio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles