25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Jukata: Sitta, Werema maadui wa Katiba

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba

Na Michael Sarungi, Dar es Salaam

JUKWAA la Katiba Tanzania (Jukata) limesema Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema ni maadui waliosababisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya kuharibika.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jukata, Deus Kibamba, alisema viongozi hao kwa nyakati tofauti kwa kutumia nyadhifa zao wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kulisababishia Taifa hasara ya mabilioni ya fedha kwa kitu wanachojua kuwa hakiwezekani.

Alisema licha ya Sitta kuelewa kuwa Bunge hilo limekosa uhalali wa kisiasa kutokana na Ukawa kususia vikao na mahudhurio duni ya wajumbe wengine na mawaziri, lakini ameziba masikio na kuendelea kusimamia vikao vyake.

Alisema pamoja na kujua kuwa Bunge limekosa uhalali wa kisheria litakapokuja katika kupata 2/3 kutoka Zanzibar wakati wa kupiga kura katika vifungu na ibara mbalimbali za Katiba, lakini amejifanya haoni na kuendelea kutafuna fedha za walipa kodi bila huruma.

Akimzungumzia Jaji Werema, alisema kiongozi huyo alijua madhara ya kisheria baada ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, kujitoa katika Kamati ya Uandishi wa Bunge lakini alishindwa kutoa ushauri wa kisheria.

Alisema kujitoa kwa Othman ni pigo kwa mustakabali wa upatikanaji wa Katiba Mpya.

“Haiingii akilini kama mwanasheria huyo anaweza kujiengua bila ya kuwa na mawasiliano na mamlaka ya uteuzi wake, kwa maana hiyo kujiengua huko kunaweza kuwa na tafsiri ya kususia kwa Zanzibar katika uandishi wa Katiba,” alisema Kibamba.

Alisema pamoja na kuzielewa athari hizo lakini hakuonekana kutoa ushauri wa maana na badala yake naye akageuka kuwa mwanasiasa kwa kuweka masilahi binafsi na kusahau majukumu yake kitaifa.

Alisema wao wanapendekeza kufanyika kwa mabadiliko ya 15 katika Katiba ya 1977 na mabadiliko ya 11 katika Katiba ya Zanzibar na marekebisho ya sheria nyingine kupitia Bunge la Muungano la Tanzania la Novemba, 2014.

- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

  1. Kibamba ulimfuata Sitta Dodoma chini ya NGO yako yenye jina la Jukwaa la Katiba.Ukaelezwa yanayoendelea Mbungeni humo ukaridhika na kusema bunge hilo linafanya kazi njema.Sasa ni wewe tena unatoa kauli tofauti Je kwanini tusiseme unawatu wanakulisha maneno?

  2. Naungana na Simon John katika maoni yake. Jukwaa la katiba hamna msimamao, mbona hampo imara katika misimamo yenu? hamjui kama mnajichanganya wenyewe na kuwachanganya wananchi? Naomba mjitfiti kuna kasoro katika utendaji wenu.NImewafuatilia mara nyingi hamtekelezi yale mnayopanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles