Sharifa Mmasi, Mtanzania Digital
Mashindano ya klabu bingwa ya mchezo wa judo nchini, yanatarajia kutimua vumbi Septemba 26-28 mwaka huu kwenye ukumbi wa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Judo Tanzania (JATA), Innocent Malya amesema lengo la mashindano hayo ni kusaka wachezaji watakaounda timu ya Taifa.
Amesema timu ya taifa itayopatikana kupitia michuano hiyo, itaingia kambini moja kwa moja tayari kwa maandalizi ya kushiriki mashindano ya Afrika Mashariki yatakayo timua vumbi mwakani nchini Uganda.
Kuhusu klabu zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ya klabu bingwa, Malya ameweka wazi na kusema kuwa mwisho wa uthibitisho ni Septemba 25,2021 baada ya hapo watatangaza orodha ya time zitakazochuana.