Damiani ni wakili kutoka nchini Uruguay, ndiye mwanzilishi wa kamati hiyo ya maadili katika shirikisho la soka, hivyo inadaiwa kwamba, kampuni yake ilifanya kazi kwa ajili ya makampuni saba ambayo yana uhusiano na Eugenio Figueredo, aliyekuwa makamu wa rais wa zamani wa shirikisho hilo na anakabiliwa na kashfa ya rushwa nchini Marekani.
Hata hivyo, Kamati ya Maadili ya FIFA inafanya uchunguzi endapo kanuni za maadili zimevunjwa, lakini Damiani amekana shutuma zinazomkabili.
“Hizi ni kashfa, lakini ukweli ni kwamba sihusiki na jambo lolote juu ya matumizi mabaya ya fedha, jambo kama hili likitokea lazima mtu utafakari na kuangalia kuna nini mbele yako.
“Kutokana na hali hii, nimeona bora niweke wazi kwamba ninajiuzulu katika kamati na kuwapisha wengine waendelee, lakini bado nawaachia nafasi ya kuendelea na uchunguzi wao kwa ajili ya kubaini ukweli,” alisema Damiani.