29.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

JPM:WASIOTAKA NDEGE WATAPATA TABU SANA

ELIZABETH HOMBO NA ANDREW NSECHU,DAR ES SALAAM


*Asema Serikali imedhamiria kutekeleza kwa vitendo miradi ya maendeleo

RAIS Dk. John Magufuli, jana aliongoza upokeaji wa ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na kusema kama wapo watu ambao hawajafurahia ujio wa ndege hiyo watapata tabu sana.

Rais Magufuli alitumia msemo huo ulioasisiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Giles Muroto alipokuwa akidhibiti maandamano ya Aprili 26, mwaka huu yaliyokuwa yakihamasishwa mtandaoni, ambapo alitoa onyo kali kwa yeyote atakayeandamana, akisema ‘watapata tabu sana,  watapata kipigo cha mbwa koko’.

Akizungumza na mamia ya wananchi waliofurika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar e Salaam jana, Rais Magufuli alisema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 262 iliyotoka moja kwa moja kiwandani nchini Marekani ni ya kisasa na anaamini Watanzania wote watakuwa wamefurahia ujio wa ndege hiyo.

“Ninaamini Watanzania wote wamefurahia ujio wa ndege hii, kama kuna watu ambao hawajafurahia ujio huu basi hao watapata tabu sana,” alisema.

Rais Magufuli alisema mafanikio ya kupatikana kwa ndege hiyo ni matokeo ya juhudi za Watanzania wote wanaojituma na kuchapa kazi, ambao wanahakikisha wanalipa kodi kikamilifu.

Alisema kwa hatua hiyo ni uthibitisho kwamba Watanzania wakiamua wanaweza, huku kiishukuru Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa kurejea na kupitisha uamuzi wa ununuzi wa ndege hiyo na nyingine tatu aina ya Bombadier ambazo tayari zimeshanunuliwa na zinaendelea na kazi nchini.

UFUFUAJI ATCL

Rais Magufuli alisema Serikali iliamua kuhakikisha inafufua Shirika la Ndege nchini (ATCL) ili kulinda heshima ya Taifa kwa kuwa ilikua ni aibu kwa nchi kutokua na ndege zake yenyewe wakati zipo nchi nyingine ndogo zisizokuwa hata na rasilimali za kutosha lakini zinamiliki ndege zao.

Alisema sababu nyingine za kununua ndege hizo ni kuimarisha na kuboresha usafiri wa ndege nchini kwa kuwa Watanzania wanahitaji usafiri wa ndege wa uhakika kwa ajili ya kusafiri wao na kusafirisha biashara zao.

habari kamili jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA hapo juu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,701FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles