24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

JPM: Wizara ya Mambo ya Nje hainifurahishi

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



Rais John Magufuli amesema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, haimfurahishi kiutendaji kazi ndiyo maana alitengua uteuzi wa Naibu Waziri wa wizara hiyo na Katibu Mkuu wake.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumamosi Septemba 29, Ikulu jijiji baada ya kumwapisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro aliyemteua wiki hii baada ya kutengua uteuzi wa Dk. Susan Kolimba.

Amesema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea wakidhani watastaafia huko kwa na kuongeza kuwa kitu kama hicho hakipo huku amkimtaka Dk. Ndumbaro kwenda kuchapa kazi.

“Wizara ya mambo ya nje haijanifurahisha sana mambo yake hayaendi vizuri sana kama inavyotakiwa inawezekana wakurugenzi wake wako ‘weak’ sana wanaona ‘business as usual’ naomba ukienda huko usije ukaungana nao.

“Wizara ile viongozi wake wanatembea sana na waziri lazima nimtume nje kutuwakilisha kuna mikutano mingi atatumwa ikiwamo pamoja na wewe, ni matumaini yangu unaenda pale utajitahidi kuifanya kazi vizuri ndiyo maana niliamua nitoe wote Naibu Waziri na Katibu Mkuu na bahati yake imepatikana nafasi, isingepatikana nafasi ya kumpeleka angetoka hivyo hivyo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles