30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

JPM: WATAKAOSHINDWA KUEDESHA VIWANDA WANYANG’ANYWE

Anna Potinus – Dar es salaam

Rais John Magufuli amewataka wamiliki wa viwanda nchini kuhakikisha wanaviendesha viwanda hivyo kwa ubora wa hali ya juu na ikitokea wakashindwa kufanya hivyo wanyang’anywe.

Rais Magufuli amesema hayo leo Alhamisi Aprili 4, wakati akizindua kituo cha afya katika kijiji cha Mbonde Wilayani Masasi Mkoani Mtwara katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo iliyoanza Jumanne Aprili 2.

Katika uzinduzi huo amemtaka Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga kuwanyang’anya viwanda wamiliki walioshindwa kuzalisha katika kiwango cha juu ambapo amesema kuwa kubinafsisha sio shida, tatizo ni kumpa mtu halafu akashindwa kukiendeleza.

“Yule wa Newala kama ameshindwa kukiendesha kile kiwanda, Waziri wa Kilimo mnyang’anye hata kama ni leo na ikishindikana mpeleke mahakamani, kuna mmoja nilimpigia simu akasema nimpe mwezi mmoja kitaendeshwa kwa asilimia 100 sasa kwa wale waliosimama tu viwanda havifanyi chochote wanyang’anyeni,” amesema

“Tukibembelezana hatutafika ndugu zangu subirini nimalize muda wangu tutabembelezana wakati wangu hakuna kubembelezana ni lazima twende kwenye mstari ulionyooka ili tuwahudumie wananchi wanaonyanyasika,” amesema.

Rais Magufuli amefungua kituo hicho kuwakilisha vituo 352 vilivyojengwa na kukarabatiwa nchi nzima vilivyogharimu bilioni 184 ambapo katika Mkoa wa Mtwara vituo ambavyo vimekarabatiwa viko saba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles