22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

JPM: SITAONDOKA MADARAKANI BILA KUPANDISHA MISHAHARA

Anna Potinus

Rais John Magufuli amewahakikishia wafanyakazi wote nchini kuwa kipindi chake cha urais hakitaisha kabla hajawapandishia mishahara.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Mei Mosi, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi ambyo kitaifa yalifanyika mkoani Iringa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya na wafanyakazi kutoka mikoa mbalimbali nchini.

“Serikali yenu inawathamini sana ndiyo maana ninawaeleza ukweli ninajua mnayoyafanya yanaleta tija hivyo naomba muamini kama miradi itaenda vizuri na uchapakazi utaendelea vizuri kipindi changu cha urais hakitaisha kabla sijawapandishia wafanyakazi mishahara,” amesema Magufuli.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amewataka wafanyakazi kuwajibika kikamilifu kwa kuwa na nidhamu ya kazi ili kukuza uchumi wa nchi.

“Nidhamu na uwajibikaji kwa wafanyakazi ni jambo la muhimu na lazima sana, mfanyakazi akiwa mzembe na mvivu anakuwa mnyonyaji kupitia mshahara anaopokea bure,” amesema Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles