24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

JPM, Museveni kuhudhuria mdahalo wa mtazamo na maono ya Mwalimu Nyerere

Asha Bani -Dar es salaam

RAIS Dk. John Magufuli na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, wanatarajiwa kuhudhuria mdahalo wa mtazamo na maono ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere kuhusu maendeleo, umoja, amani, kujitegemea kiuchumi na viwanda utakaofanyika leo Dar es Salaam.

Mdahalo huo utafanyika mara tu baada ya ufunguzi rasmi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Joseph Butiku, inaeleza kuwa Rais Magufuli na Museveni watakuwa wageni rasmi katika ufunguzi huo wa jengo ambalo lipo Barabara za Morogoro eneo linalojulikana kama MNF Square.

Alisema jengo hilo litakuwa na ofisi za Taasisi ya Mwalimu Nyerere ambazo ni utawala, maktaba itakayokuwa na nyaraka na kumbukumbu za Mwalimu Nyerere zinazohusu maendeleo, amani, umoja na mfumo wa uchumi duniani na pia chuo cha mafunzo ya uongozi.

“Pia lina eneo la takribani mita za mraba 3,600 ambazo zinapangishwa kwa ajili ya kuipatia taasisi mapato ya kujiendesha. Eneo hilo linajumuisha hoteli ya kiwango cha nyota tano ijulikanayo  kama Johari Rotana Hotel ambayo mwendeshaji wake ni Rotana Hotels Corporation ya Dubai,” alisema Butiku.

Alisema jengo hilo mmiliki wake ni Taasisi ya Mwalimu Nyerere na limejengwa kwa mkopo kwa CRJE ambayo ni kampuni tanzu ya CRJE Ltd, ambalo ni shirika la umma la China na IFC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles