29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

JPM kuruhusu michezo kuendelea

Mwandishi Wetu -Geita

RAIS wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amesema idadi ya wagonjwa wa Virusi vya Corona katika vituo vilivyotengwa imepungua sana, hivyo anaangalia uwezekano wa wiki hii kuruhusu michezo iendelee.

Akizungumza jana baada kushiriki ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT, Usharika wa Chato mkoani Geita,Magufuli alisema michezo nisehemu ya burudani kwa Watanzania hivyo lazima maisha yaendelee.


“Kwa hali hii, kama wiki tunayoianza kesho itaendelea hivi nimepanga kufungua vyuo ili wanafunzi wetu waendelee kusoma, lakini nimepanga pia kuruhusu michezo iendelee kwasababu michezo ni sehemu ya burudani, maisha lazima yaendelee.

“Ugonjwa huu wa corona ni vita kama vita nyingine, wakati unaanza nilisema siwezi kuruhusu “lockdown”, ‘imagine’(fikiri) unafungiwa ndani hupati hata nafasi ya kuonana na mkeo?, unafungiwa ndani eti usitembee usiku kana kwamba corona inatembea usiku tu, nikasema hapana,”alisema Magufuli.

Machi 17,2020 Serikali ilizuia mikusanyiko ya watu isiyo ya lazima ikiwemo michezo,ikiwa ni tahadhari ya kuepuka kusambaa kwa virusi vya corona ambavyo vimeuwa maelfu ya watu duniani. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,609FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles