21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

JPM kukutana na wafanyabiashara Ikulu leo

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli leo anatarajia kukutana na wafanyabiashara kutoka wilaya zote hapa nchini na wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC).

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais – Ikulu, Gerson Msigwa, ilieleza kuwa wafanyabiashara watano kutoka kila wilaya hapa nchini watawawakilisha wafanyabiashara wenzao.

“Mkutano huo utaanza saa 3:30 asubuhi na kurushwa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari vya redio, televisheni na youtube channel ya Ikulu – mawasiliano.

“Wajumbe wote wanatakiwa kuwasili katika ukumbi wa Kikwete kuanzia saa 2:00 hadi saa 2:30 asubuhi,” alisema Msigwa katika taarifa yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,800FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles