22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

JPM kuanza ziara Zanzibar leo

Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli amewasili Dar es Salaam akitokea nyumbani kwake Chato mkoani Geita na leo anatarajiwa kuanza ziara ya siku mbili visiwani Zanzibar. 

Katika ziara hiyo ya kikazi, anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la jengo la Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, ilieleza kuwa kesho Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari Mwanakwerekwe iliyopo Mjini Magharibi  pamoja na kufungua hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Verde Azam Luxury Resort and Spa iliyopo Mtoni.

“Mheshimiwa Rais Magufuli atashiriki sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zitakazofanyika Jumapili tarehe 12 Januari, 2020 katika Uwanja wa Amaan, Mjini Magharibi,” ilieleza taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles