26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

JPM: Chapeni kazi

Na MWANDISHI WETU

Rais Dk. John Magufuli amewatoa hofu Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwani ameanza nao na atamaliza nao.

Rais Magufuli amesema hayo leo Novemba 9, katika hafla ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

“Mkuu wa mkoa unakuwa na wasiwasi gani labda kama ulikuwa ufanyi kazi vizuri kwasababu nashangaa napata vimesji vingine Mhe Rais nimejitahidi katika kipindi changu kana kwamba kipindi chake nilimwambia kinaisha baada ya mimi kuapishwa nimeona hili nilizungumze kwamba Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya msiwe na wasiwasi” amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli amesema kuwa kunaweza kusitokee mabadiliko katika nafasi hizo isipokuwa kwa mtu anayestaafu au atakayefanya mambo ya hovyo;

 “kwanini nibadilishe Mkuu wa mkoa, kwanini nibadilishe mkuu wa Wilaya, kwanini nibadilishe Mkurugenzi, kwanini nibadilishe DAS Serikali ni ile ile” Amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli amewataka watendaji hao kuchapa kazi kwani anajua alianza nao na atamaliza nao, ameongeza kuwa hata kwa watendaji wengine akitolea mfano Makatibu Wakuu nao itakuwa hivyo hivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles