21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

JPM azindua rasmi makao makuu Dodoma, amtunuku Luteni Kanali kuwa Brigedia Jenerali

Anna Potinus

Rais Dk John Magufuli amezindua rasmi Mkoa wa Dodoma kuwa makao makuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Jumamosi Aprili 13 ambapo amewataka watumishi wote wa serikali kuhakikisha wanahamia mjini hapo hadi kufikia Jumatatu Aprili 15.

Katika uzinduzi huo uliofanyika katika eneo la Mtumba Mkoani humo Dk Magufuli amewataka wakazi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla kutumia fursa hiyo kukuza uchumi wa nchi kwa kuwekeza katika biashara mbalimbali.

“Ninawasihi watanzania kwa ujumla kutumia fursa ya serikali kuhamia Dodoma kama mlivyosikia zimetolewa ajira 1,288 na fursa bado zipo kama vile shule, hospitali, migahawa, kilimo na hoteli, mmeshaona Mabalozi wameshahamia hivyo tuzitumie hizi fursa kuleta maendeleo na kuijenga Dodoma ya kisasa,” amesema

Katika hat nyingine Dk Magufuli amempandisha cheo aliyekuwa Luteni Kanali, Charles Mbuge kuwa Brigedia Jenerali baada ya kufurahishwa na utendaji wake wa kazi katika kusimamia ujenzi wa miradi mbalimbali ya serikali ikiwemo ujenzi wa ukuta wa Mererani.

“Ninawapongeza maofisa walioshiriki kukamilisha mradi huu na Kanali Mbuge alisimamia ujenzi wa majengo mbalimbali ya serikali pamoja na ukuta wa Mererani hivyo kuanzia leo atakuwa Brigedia Jerenali sitaki kuchelewa hivyo ninataka CDF ukafanye utaratibu wa vile vinavyotakiwa kuwekwa kwenye mabega awekewe,” amesema

Hata hivyo hata za baraka za kukamilisha kumtunuku vyeo kwa nafasi hiyo ya Brigedia vikafanyika na Mbuge akatunukiwa kuwa Brigedia Jenerali kamili hap hap bele ya rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,814FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles