26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

JPM awataka wafanyakazi waendelee kupiga kazi wasitishwe na corona

 MWANDISHI WETU 

WAKATI jana wafanyakazi duniani wakishindwa kusheherekea sikukuu yao ambayo hufanyika kila mwaka Mei Mosi kutokana na janga la ugojwa wa corona, Rais John Magufuli amewataka wafanyakazi nchini kuendelea kuchapa kazi na kamwe ugonjwa huo usiwe sababu ya kurudi nyuma na kuacha kuwahudumia Watanzania. 

Sikukuu ya wafanyakazi duniani huadhimishwa kila mwaka Mei mosi na huitumia kuandamana pamoja na kuanika kero zao. 

Mwaka huu wafanyakazi wengi duniani wameadhimisha sikukuu hiyo wengi wao wakiwa hawapo makazini, wengine wamepoteza kazi, wengine wanakabiliwa na hali ngumu ya mishahara na malimbikizo na kero nyingine nyingi zilizoongezewa makali na athari za virusi vya corona. 

Katika kuadhimisha siku hiyo, jana Rais Magufuli alituma taarifa akiwapongeza na kuwatakia heri Wafanyakazi wote nchini lakini akisisitiza kuendelea kuchapa kazi. 

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, na kusaniniwa na Mkurugenzi wake, Gerson Msingwa ilimkariri Rais akisema mwaka huu sherehe za Mei Mosi hazijafanyika ili kuepusha mikusanyiko ya watu, ikiwa ni hatua muhimu ya kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19). 

Rais Magufuli alisema licha ya kwamba sherehe za Mei Mosi hazikufanyika mwaka huu, Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Wafanyakazi katika ujenzi wa Taifa na itaendelea kusimamia maslahi yao na kuboresha mazingira ya kazi. 

Amewataka Wafanyakazi nchini kuendelea kuchapakazi kwa juhudi na maarifa ili Watanzania waendelee kunufaika na huduma wanazozitoa katika maeneo yao ya kazi huku wakichukua tahadhari zote zinazoelekezwa na wataalamu juu ya kujikinga na ugonjwa wa Corona. 

“Ndugu Wafanyakazi wenzangu nawapongeza sana kwa kuchapakazi, mimi nipo pamoja nanyi na natambua kazi nzuri mnayoifanya, nawaomba katika kipindi hiki ambacho dunia inapita katika wakati mgumu wa kukabiliana na ugonjwa wa Corona, sisi tuendelee kuchapakazi, kamwe ugonjwa huu usiwe sababu ya kurudi nyuma na kuacha kuwahudumia Watanzania, mimi naamini Mwenyezi Mungu atatuvusha” alisisitiza Rais Magufuli. 

Aidha, amewapongeza Waajiri wote wa Serikali na Sekta Binafsi,na ametoa wito kwao kutotumia ugonjwa wa Corona kama kigezo cha kuwanyanyasa wafanyakazi. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles