23.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

JPM AWAPANGIA VITUO VYA KAZI MABALOZI WENGINE WATATU

Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli amewapangia vituo vya kazi mabalozi watatu aliowateua Desemba 3, mwaka jana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, mabalozi waliopangiwa vituo ni Joseph Sokoine anayekuwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Omar Yussuf Mzee anayekuwa balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Algeria na Grace Mgavano anayekwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Ladis Komba nchini Uganda aliyestaafu kwa mujibu wa sheria.

Balozi Sokoine anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Deodorus Kamala ambaye kwa sasa ni mbunge na kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika wizara hiyo.

Kabla Balozi Mzee kuteuliwa kushika nafasi hiyo, alishawahi kushika nafasi mbalimbali serukalini na mara ya mwisho alikuwa Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika awamu ya kwanza ya Rais Dk. Ali Mohammed Shein.

Kwa upande wa Balozi Mgavano, kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo alikuwa ni ofisa mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu.

Mabalozi wote waliopangiwa vituo vipya vya kazi wataapishwa leo na Rais Magufuli,  Ikulu, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles