JPM awaonya wanaonunua maeneo ya Jeshi

0
869
Rais John Magufuli

Anna Potinus- Dar es salaam

Rais John Magufuli amewaonya wawekezaji wanaonunua maeneo ya Jeshi na kuamuru zoezi hilo kuachwa mara moja na kwamba yataendelezwa kwaajili ya shuguli nyingine.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Desemba 21, 2018 katika hafla ya kuwatunuku vyeo maafisa na wakaguzi wasaidizi wa polisi iliyofanyika Kurasini Jijini Dar es salaam.

“Pamekuwa na tabia ya wawekezaji kununua maeneo ya polisi, ninasema hayo maeneo yasiuzwe tuyaache, yataendelezwa kesho au hata miaka 100 ijayo, hivyo kama mlikuwa na mipango hiyo ife msiuze hata kipande kimoja,” alisema Rais Magufuli

Aliongeza kuwa, “Pale Magereza nilitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari lakini mpaka leo hazipo, nataka niwaambie ukweli nina uvumilivu lakini kwenye masuala ya fedha huwa unanishinda.

Aidha, amesema kuwa hataki kuona askari anawekwa ndani wakati alikuwa anatekeleza wajibu wake, pia ameahidi kuwatetea askari hao siku zote huku akiwataka wamtangulize Mungu mbele katika kila wanachokifanya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here