MURUGWA THOMAS- TABORA
AHADI ya Rais Dk. John Magufuli ya kuwajengea askari polisi makazi bora mkoani Tabora imekamilika.
Akisoma risala wakati wa uzinduzi wa majengo hayo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Msabila alisema kila jengo lina nyumba mbili za makazi ambapo kila moja limegharimu Sh milioni 84.6.
Sssp Msabila alisema kuwa ujenzi wa nyumba hizo unatokana na fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta Magufuli kiasi cha shilingi bilioni 10 ambapo mkoa wa Tabora ulipata milioni 150.
Aliongeza kuwa michango toka kwa wadau ambayo ilisaidia kukamilisha ujenzi huo ni Saruji, vifaa vya umeme na maji ni zaidi ya shilingi milioni 100.
Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Mwakalukwa alitoa wito kwa wadau mbalimbali Mkoani humo kuendekea kusaidia kukamilisha majengo ya Ofisi likiwemo la kikosi cha Usalama barabarani ambayo yalianza kujengwa mwaka 2015 lakini hayakailika.
Alisema uwepo wa ofisi ya za kutosha utaongeza ufanisi katika utendaji kazi kutokana na kuwa na mazingira mazuri ya kutolea huduma kwa wananchi mbalimbali.
Naye Katibu Tawala Msaidizi ( Tamisemi ), Nathalis Linuma alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora, kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuboresha makazi ili wawe na mazingira mazuri ya kuishi na kutolea huduma kwa jamii.