24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 25, 2022

JPM atimiza ahadi yake

Na Mwandishi Wetu – Dodoma

RAIS Dk John Magufuli  jana, amewasilisha fedha za michango iliyotolewa wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Chamwino mkoani Dodoma.

Fedha hizo zimewasilishwa na Katibu wa Rais,Ngusa Samike kwa

Sheikh wa Wilaya ya Chamwino, Suleiman Abdallah Matitu muda mfupi baada ya Swala ya Adhuhuri.

Pamoja na kukabidhi fedha hizo, Rais Magufuli amewapongeza na kuwashukuru watu wote waliounga mkono na wanaoendelea kuunga mkono uchangiaji wa ujenzi wa msikiti mpya na wa kisasa.

Rais Dk. Magufuli, alisema msikiti huo utajengwa na Jeshi la Kujenga

Taifa (JKT) na ujenzi wake utaanza wiki hii. Taarifa ya Ikulu haikueleza fedha zilizokabidhiwa ni kiasi gani.

Alisema watu mbalimbali wameguswa bila kujali madhehebu ya dini waliyonayo na huo ni udhibitisho wa umoja na mshikamano walionao Watanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,160FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles