23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

JPM ateua wenyeviti wa bodi watatu, Mkuchika makatibu tawala nane

Mwandishi wetu, Dar es Salaam

RAIS John Magufuli amefanya uteuzi wa wenyeviti watatu watakaoongoza bodi za taasisi mbili za Serikali na moja ya ubia wa Serikali na sekta binafsi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, Gabriel Malata ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Airtel Tanzania Ltd ambayo serikali ina mbia. Malata ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

Pia Rais Magufuli amemteua Profesa Martha Qorro kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP). Prof. Qorro ni Profesa Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Rais Magufuli pua amemteua Prof. Joseph Buchweshaija kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST).

Katika hatua nyingine, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, amefanya uteuzi wa makatibu tawala wilaya nane na kuhamisha vituo vya kazi watatu.

Makatibu tawala walioteuliwa na viuo vyao kwenye mabano ni Michael Semindu (Mbalali), Mikidadi Nchunguye (Kigoma),  Lincoln Tamba (Mlele), Neema Nyalege (Kiteto), Estomih Kyando, (Iringa), Hoffman Sanga (Mvomero) Amin Mrisho (Mwanga) na Nicodemus Shirima (Bariadi).

Waliohamishwa vituo vya kazi ni Veronica Kinyemi anayetoka Bariadi kwenda Mkuranga, Delmina Tumaini anatoka Mkuranga kwenda Kigamboni na Rahel Mhando, anatoka Kigamboni kwenda Korogwe.

Taarifa kwa umma iliyosainiwa na Katibu Mkuu Utumishi, Dk Laurean Ndumbaro, inasema wateule hao wapya wanatakiwa kuripoti Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Februari nne ili kukamilisha taratibu za uteuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles