31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

JPM ateua viongozi uvuvi wa bahari kuu

Mwandishi Wetu -Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, akiwamo Dk. Islam Mchenga aliyeteuliwa  kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA).

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, ilinukuu taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, akisema uteuzi wa Dk. Mchenga ulianza Desemba mosi mwaka jana.

Ilisema kabla ya uteuzi huo, Dk. Mchenga alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Zanzibar.

Pia Rais Magufuli amemteua Dk. Emmanuel Sweke kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA). “Uteuzi wa Dk. Sweke umeanza Desemba mosi, 2018 na kabla ya uteuzi huo alikuwa Ofisa Utafiti wa Uvuvi Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) – Kigoma,” ilisema.

Ilisema pia Rais Magufuli amemteua Profesa Sebastian Chenyambuga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa Profesa Chenyambuga ulianza Januari mwaka huu.

Taarifa hiyo inasema pia Rais Magufuli amemteua Profesa Justinian Ikingura kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania. Uteuzi wa Profesa Ikingura ulianza Januari 18.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles