29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

JPM ATEUA KAMATI NYINGINE KUCHUNGUZA MCHANGA

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli, ameteua kamati nyingine itakayofanya uchunguzi wa madini yaliyomo kwenye mchanga ulio ndani ya makontena katika maeneo mbalimbali nchini.

Kamati hiyo inayojumuisha wachumi na wanasheria imetanguliwa na kamati ya awali iliyoteuliwa Machi 29 mwaka huu ikijumuisha wataalamu wa jiolojia, kemikali ambao watafanya  uchambuzi wa kisayansi kuhusu mchanga huo.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi  iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, iliwataja wajumbe wa kamati hiyo mpya kuwa ni Profesa Nehemiah Osoro, Profesa Longinus Rutasitara, Dk. Oswald Mashindano na Gabriel Malata.

Wengine wanaounda kamati hiyo ni Casmir Kyuki, Butamo Philip, Usaje Usubisye na Andrew Massawe.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa wajumbe hao wataapishwa na Rais Dk. Magufuli saa 3:00 asubuhi  leo Ikulu Dar es Salaam.

Kamati hiyo imeundwa siku 13 tangu kuteuliwa kwa kamati nyingine iliyopewa jukumu la kuchunguza kiwango cha madini kilichomo katika makontena ya mchanga wa madini yaliyozuiliwa bandarini.

Kamati ya awali inawajumuisha, Profesa Abdulkarim Mruma ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Profesa Justianian Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dk. Yusuf Ngenya, Dk Joseph Philip, Dk Ambrose Itika, Mohamed Makongoro na Hery Gombela.

Uteuzi wa kamati hiyo ulifanyika siku chache baada ya Rais Dk. Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo pamoja na mambo mengine, Rais Dk Magufuli alipiga marufuku usafirishaji wa mchanga huo unaodaiwa kuwa na kiwango kikubwa cha madini ya dhahabu kwenda nje ya nchi kuanzia Machi 2, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles