24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

JPM: ASIYEFANYA KAZI ASILE, ASIPOKULA AFE

 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Rais John Magufuli, leo ameweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge), reli ya kati kutoka Morogoro-Makutupora-Dodoma na kuahidi ajira zaidi wakati wa ujenzi wa reli hiyo huku akisema asiyefanya kazi asile na asipokula afe.

Amesema ajira 30,000 za moja kwa moja na 600,000 zisizo za moja kwa moja wakati zitatolewa wakati wa ujenzi wa reli hiyo.

“Suala la ajira tumelijibu kwa vitendo kwa kuwa na miradi mikubwa kama hii, kinachotakiwa msichague kazi nitashangaa sana kama mkandarasi wa hapa Ihumwa akianza ujenzi watu wa hapa hamtakuja kufanya kazi na kutengeneza mapesa, asiyefanya kazi na asile na asipokula afe,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo, Rais Magufuli amesema usafiri wa reli hiyo mpya utarahishisha biashara kati ya nchi jirani ambapo pia itasaidia kutunza barabara zetu kwani mikoa mingi tayari imeunganishwa kwa barabara za lami ambazo zimekuwa zikiharibika mapema kutokana na magari makubwa ya mizigo.

“Reli hii itasaidia si tu kutunza barabaza zetu bali kuondoa gharama za kukarabati mara kwa mara kwani reli hii ina uwezo wa kubeba zaidi ya tani 100 sawa na malori zaidi ya 20,” amesema.

Amesema Tanzania imeanza kuwa nchi ya mfano kutokana na tafiti ambazo zimethibitisha usafiri wa reli ni salama zaidi kulinganisha na anga na usafiri mwingine na usalama wa mizigo.

“Ujenzi huu wa reli ya kisasa utaiongeza tija katika usafiri wa reli ambapo faida ya kwanza ni kurahisisha usalama wa mizigo na abiria, kwa sasa mtu anaweza kusafiri kutoka Dodoma hadi Dar es Salaam kwa saa tatu tu wakati wastani usafiri wa gari ikiwa ni saa tano hadi nane kwa basi.

“Tanzania tuna bahati tumefika milioni 55, wanasema kwa nini tuko wengi tunazaana sana, mimi nasema tuzaane sana, tusiogope kuwa wengi, tukubali kuwa wengi lakini wanaochapa kazi tusipochapa kazi tutalia,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles