22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

JPM amtumbua kigogo viwanja vya ndege

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli,  amemteua   Julius Ndyamukama kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, ilieleza kuwa Ndyamukama anachukuwa nafasi ya Richard Mayongela ambaye uteuzi wake umetenguliwa na ametakiwa kuripoti Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambako atapangiwa kazi nyingine.

Kabla ya uteuzi huo, Ndyamukama alikuwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam, na ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa ujenzi wa majengo namba 3  ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  Dar es Salaam ambayo yapo katika hatua za mwisho kukamilika. Uteuzi huo wa Ndyamukama ulianza jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,415FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles