JPM amteua Massawe kukaimu NIDA

Andrew Massawe
Andrew Massawe
Andrew Massawe

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais Dk. John Magufuli, amemteua Andrew Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Kabla ya uteuzi huo Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu Tanzania (BOT).

Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilieleza  Massawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Modestus Kipilimba ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here