25.7 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

JPM amteua Dk. Ng’umbi kuongoza Taasisiya Elimu

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli amemteua Dk. Michael Ng’umbi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).

Taarifa iliyotolewa jana na Ikulu ilieleza kuwa kabla ya uteuzi huo Dk. Ng’umbi alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania – OUT)

Dk. Ng’umbi amechukua nafasi ya Dk. Fidelice Mafumiko ambaye ameteuliwa kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Jaji Stephen Magoiga kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal – FCT)

Jaji Magoiga amechukua nafasi ya Mhe. Jaji Barke Mbaraka Sehel ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hawa umeanza Februari 19, 2019.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,897FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles