20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

JPM amrudisha kazini OCD Njombe baada ya maombi ya mchungaji

Bethsheba Wambura

Muda mfupi baada ya kusimamishwa kazi na Rais Dk. John Magufuli Mkuu wa Polisi Wilaya Njombe (OCD), SSP Sifaeli Pyuza amerudishwa kazini baada ya mchungaji aliyeombwa na Rais kufanya sala ya toba kuombea mauaji ya watoto yaliyokuwa yakitokea mkoani humo miezi michache iliyopita.

Hatua hiyo ya Rais Magufuli kumsimamisha na kumrudisha kazini OCD huyo imefikiwa leo Aprili 10, alipokuwa akihutubia wananchi wa mkoa wa Njombe katika muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo.

Rais Magufuli ambaye kabla ya kufikia hatua hiyo alihoji kama OCD wa eneo hilo bado yupo ilihali aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa huo (RPC) akiwa amesimamishwa kazi kwa kushindwa kumaliza mauaji ya watoto kwa wakati.

“Nilimtimua RPC hapa kwa ajili ya mauaji yaliyokuwa yanatokea hapa Njombe, OCD wa hapa bado yupo? Sasa kuanzia leo nasema naye aondoke najua ananilinda hapa lakini naye aondoke haiwezekani waletwe askari kutoka sehemu zingine kufanya operesheni wao wapo tu hapa,” amesema.

Lakini akiwa katika hotuba yake Rais Magufuli akamuita mmoja wa wachungaji aliyekuwapo katika mkutano huo wa hadhara na kumuomba aongoze sala ya toba kuombea mauaji ya watoto yaliyokuwa yakitokea mkoani humo na baada ya maombi hayo akasitisha kumtimua kazi OCD huyo.

“Haya sas wote tumekuwa wasafi na OCD niliyemsimamisha kazi nimemsamehe na atabaki kufanya kazi hapa,” amesema huku watu wakishangilia na wengine kushangazwa.

Aidha Rais Magufuli ametoa onyo endapo mauaji hayo yatatokea tena mkoani humo atawaondoa viongozi wote wa mkoa huo, “Siku nyingine mauaji yakitokea hapa Njombe RC, DC, RAS mnaondoka na hata kama kuna sijui mwenyekiti wa kijiji, mwenyekiti na katibu wa CCM mnaondoka wote ili kusudi hali kama hiyo isijitokeze tena,” amesema Dk Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles