JPM amlilia mtangazaji Marin wa TBC

0
814

Mwandishi Wetu

Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha mtangazaji maarufu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Marin Hassan Marin kilichotokea leo Jumatano Aprili Mosi katika Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam

Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema alimfahamu marehemu Marine kama mtu aliyetoa mchango mkubwa katika ustawi wa uandishi wa habari nchini na kwa juhudi zake kubwa ndani ya TBC ambapo aliripoti habari kwa ubunifu na mvuto wa hali ya juu.

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko taarifa za kifo cha ghafla cha mtangazaji maarufu na mahiri, Marin Hassan kilichotokea leo jijini Dar es Salaam.

“Marin Hassan aliipenda kazi yake ya uandishi wa habari, aliifanya kwa weledi wa hali ya juu, alikuwa mzalendo wa kweli na alidhamiria kuitumikia nchi yake kupitia chombo cha habari cha taifa kwa nguvu na juhudi zake zote.

“Marin ameondoka wakati ambao tunamuhitaji zaidi, ni shujaa wa habari Tanzania, aliipenda sana TBC na nchi yake. Naungana na familia yake, TBC na waandishi wa habari wote kumuombea apumzike mahali pema peponi,” amesema Rais Magufuli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here