30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

JPM AMKUMBUKA NUNDU, AAPISHA MABALOZI

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM


RAIS Dk. John Magufuli, amemteua Omary Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Nundu   alikuwa Mbunge wa Tanga Mjini na Waziri wa zamani wa Miundombinu wa Serikali ya Awamu ya nne ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na kusainiwa na Kurugenzi ya Mawasiliano Rais Ikulu, ilieleza kuwa uteuzi wa Nundu umeanza Februari 24, mwaka huu.

Omary Nundu anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Profesa  Tolly Mbwete.

Wakati huo huo, Rais Dk. Magufuli amemuapisha Thobias Andengenye kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Andengenye anachukua nafasi ya Kamishna Jenerali Pius Nyambacha ambaye amestaafu.

Pia Rais Dk. Magufuli amewaapisha mabalozi wanne walioteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali ambako Dk. Pindi Chana ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya kuchukua nafasi ya John Haule ambaye amestaafu.

Silima Kombo Haji ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Khartoum, Sudan ambako anakwenda kufungua Ubalozi huku Abdallah Abas Kilima akiapishwa kuwa Balozi wa Tanzania, Muscat, Oman ambako anachukua nafasi ya Ali Ahamed Saleh aliyestaafu.

“Matilda Masuka ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Seoul, Korea Kusini   anakokwenda kufungua Ubalozi mpya.

 “Rais Dk. Magufuli pia alishuhudia Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Mabalozi wote wanne wakila kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela,” ilieleza taarifa hiyo ya Ikulu

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao ilihudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles