JPM aitaka ATCL kupunguza matumizi

0
1805

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Rais Dk. John Magufuli, amelitaka Shirika la Ndege nchini (ATCL) kupunguza gharama za uendeshaji zisizo za msingi.

Ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 11, alipokuwa akihutubia viongozi mbalimbali na umati wa wananchi wa jiji la Dar es Salaam waliofurika katika Uwanja wa Ndege wa zamani (Terminal 1) katika mapokezi ya ndege mpya iliyotua leo ya Airbus 220-300 Ngorongoro.

“Mpunguze matumizi ya hovyo, mhakikishe kila biashara mnayofanya iwe na faida hatutaki biashara za hasara hapa, na mjue ndege hizi tumewaazima mkileta mzaha tutawanyang’anya.

“Kuna wakati ndege za ATCL  zilikuwa zinaenda Dubai ila kumbe zikienda kule zinaenda kufuata nguo za maduka ya watu fulani fulani,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amewataka watumishi wa shirika hilo wakiwamo marubani na wafanyakazi wa ndani wa ndege kufanya kazi kwa uadilifu ili kulisaidia shirika hilo kuendelea kukua.

“Ombi langu kwa wafanyakazi wa ATCL mfanye kazi kwa moyo na uadilifu mkubwa na muwahudumie abiria kwa upendo ili waendelee kutumia ndege zenu, tunataka tushindane na mashirika mengine duniani kwasababu watu wa kutufikisha huko wapo,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here